Maafisa wa afya huko Haiti wanasema mlipuko wa kipindupindu unasamba nchini kukiwepo zaidi ya watu 4,100 waloambukizwa na 292 wamefariki.
Naibu mkurugenzi wa shirika la Afya la nchi za Amerika, PAHO, Jon Andrus aliwambia waandishi habari mjini Washington Jumatano kwamba milipuko wa kipindupindu ungali umebaki katika maeneo ya kaskazini na kati ya nchi.
Andrus anasema wizara ya afya ya Haiti kwa kushirikiana na PAHO na mashirika mengine ya Umoja wa Matiafa imebuni mkakati wa kuzuia ugonjwa huo kuenea na kuwatibu waloambukizwa.
Anasema mpango ni pamoja na kusambaza paketi za mchanganyiko wa chumvi na sukari inayotumiwa kutibu na kuzia matatizo yanayotokana na ugonjwa wa kipindupindu anasema Andrus.