Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 01:12

Mlinda amani wa UN raia wa Tanzania auwawa Congo


Baadhi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Congo
Baadhi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Congo

Tume ya Umoja wa Mataifa-UN nchini Congo inasema mlinda amani mmoja ameuwawa kufuatia mapigano katika eneo la Beni kwenye jimbo la Kivu kaskazini nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP tume hiyo ilisema Jumatatu kwamba mlinda amani huyo raia wa Tanzania alipigwa risasi wakati wa shambulizi la Jumapili lililofanywa na washukiwa waasi wa kundi la Allied Democratic Forces kwenye eneo la vikosi vya jeshi.

Ilisema eneo la jeshi lilikuwa kiasi cha mita 500 kutoka kwenye kituo cha Umoja wa Mataifa. Tume ya Umoja wa Umoja ilisema mlinda amani mwingine raia wa Tanzania alijeruhiwa katika mapigano na amehamishiwa kwenye hospitali ya Umoja wa Mataifa huko Goma.

Antonio Guterres, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Antonio Guterres, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alilaani mauaji hayo na aliisihi serikali ya Congo kuchunguza tukio hilo na kuwafikisha waliohusika mbele ya sharia. Katika taarifa yake aliyataka makundi yote yenye silaha nchini Congo kusitisha ghasia.

XS
SM
MD
LG