Mkuu wa zamani wa wafanyakazi katika jeshi la Burkina Faso ambaye alifutwa kazi mwezi Oktoba ametekwa nyara kutoka nyumbani kwake na “watu wasiojulikana waliokuwa na silaha”, vyanzo karibu naye vimesema Jumatatu.
“Walifunga kitongoji, wakaizingira nyumba yake kabla ya kumchukua,” chanzo cha usalama kilicho karibu na mkuu huyo wa zamani wa polisi kiliiambia AFP. Luteni kanali Evrard Somda alichukuliwa Jumapili kutoka nyumbani kwake katika mji mkuu, Ouagadougou, aliongeza.
“Hatujui kama ni kukamatwa kwa amri ya jeshi au mamlaka ya mahakama, au kama ni utekaji nyara mwingine,” chanzo kingine karibu na Somda kilisema. Somda alifutwa kazi wiki moja baada ya maafisa wanne wa polisi kukamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika njama dhidi ya usalama wa taifa ambapo utawala wa kijeshi ulisema ulizuia.
Afisa huyu aliyeheshimika, Somda alikuwa katika wadhifa huo tangu Februari 2022 lakini aliona nafasi yake ikidhoofishwa kutokana na kukamatwa kwa maafisa hao wanne, ambapo walikuwepo washirika wake wawili wa karibu.
Forum