Sidibe alitangaza uamuzi huo jana baada ya mkutano wa siku tatu wa bodi ya UNAIDS uliokua unazungumzia ripoti ya jopo maalum inayoeleza kwamba chini ya uongozi wake ameruhusu tabia ya unyanaysaji wa kingono, uonevu na utumiaji mbaya wa madaraka.
Jopo la wajumbe wanne ilitayarisha ripoti ya kurasa 70 inayoeleza kwamba mila ya mfumo dume katika utawala huo ina upendeleo na kuwaajiri marafiki na ndugu, na kuwa hakuna uwajibikaji na kuna vitendo vya ulipizaji kisasi.
Sidibe raia wa Mali, amekuwa mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo tangu 2009, liloajiri wafanyakazi 670 kote duniani lenye makazi yake mjini Geneva .
Sidibe amenukuliwa akisema katika taarifa ya UNAIDS akisema kwamba “Nitafanya kazi kuhakikisha kuna kipindi kizuri cha mpito na naahidi kuzingatia maslahi ya wafanyakazi wetu na kutoa matokeo chanya kwa watu tunaowatumikia.”
Umoja wa Matiafa umejaribu mnamo miaka ya hivi karibuni, kuimarasha hali ya uwazi na jinsi inavyokabiliana na tuhuma muhimu, baada ya mfululizo wa mashtaka ya unyanyasaji wa kingono na dhulma dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.