Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 03:35

Mkuu wa jeshi la Marekani: jeshi la China ni tishio kwa usalama wa Marekani na washirika wake


Mkuu wa jeshi la Marekani, Jenerali Mark Milley akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini Stockholm, June 4, 2022. Picha ya Reuters
Mkuu wa jeshi la Marekani, Jenerali Mark Milley akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini Stockholm, June 4, 2022. Picha ya Reuters

Jeshi la China limekuwa tishio na hatari zaidi katika miaka mitano iliyopita, mkuu wa jeshi la Marekani alisema wakati wa ziara yake katika kanda ya Indo-Pacific akianza na ziara hiyo Jumapili nchini Indonesia.

Jenerali Mark Milley, alisema idadi ya mawasiliano ya wanajeshi wa Marekani na washirika wengine yanayonaswa na ndege na meli za China katika eneo la Pacific imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi hicho, na idadi ya mwingiliano usio salama imeongezeka kwa viwango kama hivyo.

“Ujumbe ni kwamba jeshi la China, angani na baharini, limekuwa tishio kubwa na la dhahiri katika eneo hili,”, alisema Milley, ambaye hivi karibuni aliwaomba wafanyakazi wake kukusanya maelezo juu ya mwingiliano kati ya China na Marekani na washirika wengine katika kanda hiyo.

Matamshi yake yanajiri wakati Marekani imeongeza maradufu juhudi za kuimarisha uhusiano wake na mataifa ya kanda ya Pacific kama njia ya kukabiliana na China, ambayo inajaribu kuongeza uwepo wake na ushawishi wake katika eneo hilo.

Utawala wa Biden unachukulia China kama “tishio la haraka” na changamoto kuu ya muda mrefu ya usalama wa Marekani.

XS
SM
MD
LG