Mkuu wa FBI anasema Marekani inakabiliwa na vitisho kutoka sehemu nyingi wakati ambapo idara za usalama zinajitahidi.
Mkurugenzi wa FBI Christopher Wray anasema “ana wakati mgumu kufikiria muda katika taaluma yangu ambapo kuna aina nyingi tofauti za vitisho vyote vimeongezeka mara moja”.
Wray alizungumza Jumatano katika mahojiano maalum na shirika la habari la Associated Press wakati alipotembelea ofisi ya shirika lake huko Minneapolis kuzungumzia ushirikiano kati ya idara za usalama na pia na taasisi nyingine.
Matamshi yake yanakuja wakati FBI inakabiliana na wasiwasi mkubwa juu ya ugaidi wa ndani na wa kimataifa, pamoja na ujasusi wa China na wizi wa miliki na uingiliaji kati wa nje katika uchaguzi.
Forum