Nchini Tanzania kumefanyika mkutano mkubwa wa uwekezaji unaojumuisha nchi za afrika mashariki.
Mkutano huo wa siku mbili uliofunguliwa jumatatu unajumuisha viongozi mbalimbali kutoka afrika mashariki akiwemo rais Yoweri Museveni wa Uganda, rais Mwai Kibaki wa Kenya na mawaziri mbalimbali pamoja na wakurugenzi wan chi za nje.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania aliufungua rasmi mkutano huo wenye lengo la kuwakutanisha wawekezaji kujadili masuala muhimu hasa ya uwekezaji na kibiashara.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji bwana Ole Naiko ambaye kituo chake ndicho kimesimamia mkutano huo amesema mara baada ya mkutano huo wadau watapata nafasi ya kukubaliana na kuingia katika mikataba mbalimbali ya uwekezaji.
Amesema hii fursa nzuri kwa Tanzani ambayo inasifika ulimwenguni kwa kuwa na amani nchi mwake lakini vilevile hivi sas aitapata nafasi ya kujitangaza zaidi katika mwelekeo wa vivutio muhimu ilivyonavyo kama vile utalii .
Amepongeza makampuni mbalimbali yaliyojitokeza kudhamini mkutano huo pamoja na wananchi walijitokeza kwa wingi kushiriki.