Kuendesha gari katika jiji la New York siku zote ni tukio lisilo la kawaida, huku magari yakigongana na wapiti njia wakijitahidi kupata njia ya kupita katika barabara za mji na sehemu za watembea kwa miguu.
Zaidi ya wakazi milioni moja na nusu wanaishi Manhattan, pia ni makao mkuu ya Umoja wa Mataifa. Kuendesha gari jiji hilo kunataka ustadi wa aina yake kwasababu mara nyingine utahisi kama ni jinamizi, lakini katika kipindi hiki cha wiki mbili katika mwezi huu wa Septemba wakati wa kikao cha kila mwaka cha Baraza Kuu la Umoja wa mataifa, magari barabarani yanakumbana na ulinzi mkali kwasababu ya wakuu wa serikali takriban 193 wanaohudhuria kikao hicho.
Fikiria pale unapokuwa katikati ya barabara. Magari yameshonana barabarani yakitembea kwa mwendo wa pole pole.
Magari ya polisi nayo yako jirani kabisa. Hakuna anaweza kufika sehemu yoyote kwa haraka zaidi wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Labda uwe ndani ya moja ya magari 200 yanayowaendesha waheshimiwa kwenda na kutoka Umoja wa Mataifa.
Sajenti Patrick McGuire wa idara ya polisi New York, anayehusika na usalama kwa ajili ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa anasema, “kuna watu wa idara ya usalama, wale wa idara ya polisi na wa upelelezi ambao wanayakagua magari yanayoingia katika eneo hilo.”
Baada ya shughuli hiyo ndipo wanapoweza kuingia ndani. Kwenda Umoja wa Mataifa kunaanzia kwenye kituo cha operesheni. Idara ya ulinzi wa kidiplomasia kwenye Wizara ya Mambo ya Nje imechukua ghorofa nzima katika hoteli ya Midtown.
Eneo hilo limeandaliwa katika muda wa saa 72 lakini inachukua miezi minane ya kupanga. Watu elfu moja na magari zaidi ya 100 yenye kubeba silaha na magari aina ya aina yake aina ya Limousine ambayo yanasimamiwa na kikosi maalum kinachojulikana kama “Swat Team” na magari mengine pia kwa ajili ya waheshimiwa.
J. R. Kulik, mratibu wa idara ya usalama kwa ajili ya Baraza Kuu la Umoja wa mataifa anasema “wafanyakazi wetu wanafanya kazi katika maeneo haya husika kwa ajili ya ulinzi na kuwaweka salama wale wanaolindwa na kwa kweli ni kazi ya aina yake kwasababu muda wote wako katika harakati.
Lazima tuhakikishe kwamba tunadhibiti ulinzi katika kila upande, bila ya kujali wanakwenda wapi na muda gani katika na sehemu gani.”
Idara ya Usalama ya Marekani inashughulika na viongozi wa serikali kama marais na mawaziri wakuu.
Msafara wa magari unavyokuwa mrefu, na kiwango cha tishio kwa kiongozi kinakuwa kikubwa. Fikiria dhamana ya usalama kwa Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan. Ghorofa ya 40 ya ubalozi wa Uturuki iliyofanyiwa ukarabati mpya ikoa mkabala kutoka Umoja wa Mataifa, ambako baadhiya maafisa wanaliita ni jinamizi la ulinzi.
Kishore Mirchandani ambaye anaishi katika mtaa wa 45 mkabala na Umoja wa Mataifa kwa takriban miaka 15 anasema, “ kwa mfano, kama nahitaji kwenda kucheza gofu kesho. Kwahiyo, vifaa vyangu vya gofu naviacha kwa rafiki yangu mtaa wa 65.”
Toshie Deuskar, mkazi wa New York, anasema akitembelea hakuna tatizo. Tatizo linakuwa pale anapoamua kuwa ataendesha gari yake.
Kwa mipango yote hiyo na zamu ya saa 12, unaweza kufikria kuwa polisi wa jiji la New York huenda wakapata walau mapumziko baada ya wiki hii.
Sajenti Patrick McGuire wa idara ya polisi ya New York anayehusika na ulinzi wa UNGA, “tulianza kupanga tukio letu jingine lijalo mara moja. Huko Manhattan, siku zote kuna kituo kinachotokea.”
Fikiria msururu wa magari barabarani ulivyo katika barabara za jiji la New York kipindi hiki cha UNGA.