Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 11:53

Mkutano wa WTO wafunguliwa Nairobi

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Kenya Amina Mohamed na Mkurugenzi mkuu wa WTO Roberto Azevedo mjini Nairobi
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Kenya Amina Mohamed na Mkurugenzi mkuu wa WTO Roberto Azevedo mjini Nairobi

Zaidi ya wajumbe 7,000 wanahudhuria mkutano huo wa WTO ambao washiriki wengi walianza kuwasili mjini Nairobi , Kenya tangu wiki iliyopita kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huo.

Mkutano wa 10 wa mawaziri wa nchi wanachama wa shirika la biashara duniani, WTO umefunguliwa rasmi mjini Nairobi Jumanne huku Rais Ellen Johnson wa Liberria akiongoza mkutano wa wafanya biashara wanawake duniani.

Zaidi ya wajumbe 7,000 wanahudhuria mkutano huo wa WTO ambao washiriki wengi walianza kuwasili mjini Nairobi , Kenya tangu wiki iliyopita kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huo.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ndiye aliyefungua rasmi mkutano huo unaofanyika katika jumba la mikutano la KICC na kuhudhuriwa na wajumbe elfu 7,000 -,wengi wao kutoka mataifa yanayoendelea.

Rais Ellen Johnson Sirleaf akihutubia mkutano wa Wanawake WTO Nairobi
Rais Ellen Johnson Sirleaf akihutubia mkutano wa Wanawake WTO Nairobi

Kabla ya sherehe hizo, Ellen Johnson Sirleaf aliongoza mkutano wa wafanyi biashara 350 wanawake kutoka sehemu mbali mbali duniani wakiwemo wengi pia kutoka nchi za Afrika.

Naye naibu wa rais wa Kenya William Ruto, alitoa wito kwa mashirika ya fedha kutoa mikopo nafuu kwa wafanyi biashara wanawake ili kushiriki kikamilifu katika ustawi wa uchumi na maendeleo kwa jumla.

Baadhi ya washiriki katika mkutano huo wamesema unamanufaa kwa sababu pia unatoa fursa ya kubadilisha mawazo, uzoezfu n ahata mbinu za kibiashara kutoka taifa moja kwenda lingine. Lakini wakulima wa majani chai, kahawa na bidhaa nyingine za kilimo wana mashaka ikiwa watafaidika na matokeo ya mkutano huo.

XS
SM
MD
LG