Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:19

Mkutano wa Uingereza wakubaliana juu ya mkataba wa Somalia


Mkutano wa Kimataifa kuhusu Somalia nchini Uingereza
Mkutano wa Kimataifa kuhusu Somalia nchini Uingereza

Washirika wa kimataifa wamefikia makubaliano juu ya mkataba wa usalama wa Somalia na hatua mbali mbali za maboresho nchini humo.

Mkutano huo uliofanyika Uingereza umewaleta pamoja viongozi kutoka nchi mbalimbali duniani.

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya Uingereza katika Umoja wa Mataifa mkutano huu umekuwa ni chachu katika kuboresha sekta ya usalama, kujenga uwezo wa kimataifa katika kukabiliana na ukame na majanga ya kibinadamu yanaendelea kujitokeza nchini Somalia.

Pia nchi hizo kwa pamoja zimekubaliana kuwa na ushirikiano wa kimataifa unaohitajika kuifanya Somalia iwe katika mwelekeo wa amani na mafanikio ifikapo 2020.

Mkutano huu ulifunguliwa na Waziri Mkuu Theresa May Alhamisi. Waliokuwa wazungumzaji wakuu ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Boris Johnson, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa Priti Patel, Waziri wa Ulinzi Sir Michael Fallon, Rais Farmajo wa Somali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Guterres na Mwenyekiti Faki wa Umoja wa Afrika.

Mkutano huo pia uliangaza juu ya makubaliano ya mkataba wa Usalama, uliokubaliwa na Somalia na jumuiya ya Kimataifa, ambao utaruhusu mwendelezo na usalama wa muda mrefu wenye majukumu yaliyokubaliwa na pande zote.

Uingereza inaisaidia Somalia kujenga utulivu kupitia shirika lake la misaada UKAid, ikiwa imejikita katika kujenga taifa la Somalia, kuifanya serikali iwe imara na kuzisaidia taasisi kuwa ni zenye kutekeleza majukumu yake na kuwajibika ipasavyo. Aidha imepeleka wanajeshi wake 70 ambao wanalisaidia jeshi la Somalia.

Uingereza inaongoza katika kutoa misaada ya majanga ya kibinadamu huko Somalia, kwa kuwapatia chakula, maji na madawa watu zaidi ya milioni moja.

XS
SM
MD
LG