Rais wa zamani wa marekani, Bill Clinton ameyataka mashirika ya misaada kuhusu ukimwi kutumia kwa vizuri na uangalifu michango wanayopewa na mataifa tajiri. Bwana Clinton alizungumza hivi leo kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu ukimwi huko Vienna. Rais wa zamani aliyaambia makundi ya ukimwi kwamba taasisi nyingi zinatumia fedha nyingi kupeleka wafanyakazi kuhusu masuala ya ukimwi kwenye mikutano na shughuli nyingine. Amesema kila dola inayotumiwa inayaweka maisha ya mtu hatarini. Amesema hali ya uchangishaji fedha zaidi hapo baadae kwa ajili ya kazi za ukimwi kwa kiasi kikubwa itategemea kiwango cha michango midogo midogo inayofanywa watu wengi zaidi. Alielezea mfano wa kuchangisha fedha kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi la mwezi January huko Haiti.
Rais wa zamani wa marekani, Bill Clinton ameyataka mashirika ya misaada kuhusu ukimwi kutumia kwa vizuri na uangalifu michango wanayopewa na mataifa tajiri.