Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 16:10

Mkutano wa Francophone wazungumzia mzozo wa Mali na DRC


Rais wa DRC Joseph kabila (L) na Rais wa Ufaransa Francois Hollande kwenye mkutano wa Francophone huko Kinshasa, Oct. 13, 2012.
Rais wa DRC Joseph kabila (L) na Rais wa Ufaransa Francois Hollande kwenye mkutano wa Francophone huko Kinshasa, Oct. 13, 2012.
Marais kutoka nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa wamemaliza mkutano wao Kinshasa, huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC kwa kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuwawekea vikwazo viongozi wa kundi la waasi la M23 ambalo linahusika na machafuko na visa vya uhalifu mashariki mwa DRC.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:47 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Sauti ya Amerika ilizungumza na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo ambaye anaanza kuelezea kuhusu azimio la viongozi hao katika mzozo wa kaskazini mwa Mali.

Viongozi hao kutoka nchi wanachama wa Francophone walikubaliana pia katika azimio la pamoja kuitaka Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi – ECOWAS kupeleka jeshi maalum ili kukabiliana na uasi wa wanamgambo wa kiislamu kaskazini mwa Mali.

Katika azimio lao la pamoja wameisihi ECOWAS kuharakisha kupeleka jeshi kaskazini mwa Mali na kuomba hilo lifanyike katika kipindi cha siku 45.

Pia katika azimio lao viongozi hao walielezea umuhimu wa kuwepo na uwazi katika taratibu za uchimbaji madini na biashara ya rasilimali za kitaifa katika nchi wanachama na haja ya kusisitiza matumizi bora ya misitu kwa ajili ya hifadhi ya mazingira.

Mkutano mwingine wa Francophone unatarajiwa kufanyika baada ya miaka miwili na utawakutanisha viongozi hao Dakar, Senegal.
XS
SM
MD
LG