Mkutano wa hapo awali wa Baraza jipya la NATO na Ukraine unaotarajiwa kushughulikia usalama wa Black Sea umepangwa kufanyika Jumatano Rais Volodymyr Zelenskyy alisema katika hotuba yake Jumapili usiku.
Msemaji wa NATO Oana Lungescu alisema Jumamosi kwamba mkutano huo ulioombwa na Zelenskyy katika mazungumzo ya simu na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg utajadili hali hiyo kufuatia kujiondoa kwa Russia katika mkataba wa mwaka mmoja wa kusimamia mauzo ya nafaka kutoka bandari za Ukraine.
Kwa hakika tarehe ilikubaliwa mara tu baada ya mazungumzo yetu jana Zelenskyy alisema. Mkutano utafanyika Jumatano hii.
Aliongeza kusema kwamba mkutano huo ni miongoni mwa matukio ambayo Ukraine inajiandaa kwa ajili ya wiki ijayo ambao utaimarisha ulinzi wa nchi hiyo. Alisema misaada mipya inatayarishwa ikiwa ni pamoja na ulinzi zaidi wa anga mizinga na silaha za masafa marefu.
Forum