Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 03:00

Mkutano wa AU, Afrika Kusini.


Viongozi wa mataifa ya Umoja wa Afrika ,AU kwenye picha ya awali.

Mkutano wa 25 wa Umoja wa Afrika (AU) unaendelea nchini Afrika Kusini, huku viongozi wakitarajiwa kulenga masuala ya changamoto za usalama kote barani humo, suala la wahamiaji wanaovuka bahari ya Mediterranean na kuboresha miundo mbinu.

Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Maite Nkoana Mashabane amesema nchi yake imefanya mipango yote kwa mkutano utakaokuwa na mafanio wa Umoja wa Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Pretoria Jumatatu, amesema kutokomeza umaskini ni suala lililo juu katika ajenda.

“Itahitaji nia zetu kufanya juhudi zaidi, hasa kwa kizazi cha vijana na kufanya kazi kwa ajili ya mafanikio ya bara hili na kutokomeza kabisa umaskini kwa kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi katika mikono yetu wenyewe', amesema waziri Mashabane.

Bara la Afrika linakua haraka mno. Nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi ya haraka hapa duniani ziko katika bara hilo. Lakini wataalamu wanaamini kuwa ukosefu wa barabara nzuri, njia za ugavi umeme na miundo mbinu mingine inadumaza ukuaji.

Elham Ibrahim, Kamishna wa AU kwa masuala ya miundo mbinu na nishati amesema suala hili pia litapewa mtizamo mkubwa kama sehemu ya ushirika mpya kwa program ya maendeleo na ushirikiano wa kiuchumi Afrika katika AU (NEPAD).

Ghasia za kisiasa nchini Burundi na vita huko Sudan Kusini ni mambo ambayo yatajadiliwa katika mkutano. Viongozi pia wataangalia kwa kina zaidi kuendelea kwa vitisho vya kigaidi katika nchi kama vile Kenya, Nigeria na Somalia.

Mkutano wa AU utamazilika kwa kikao cha wakuu wa nchi kitakachofanyika June 14 na 15.

XS
SM
MD
LG