Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 28, 2020 Local time: 09:13

Trump kuzungumza na waandishi wa habari


Rais mteule, Donald Trump akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Trumo Tower huko New York, Desemba 6, 2016.

Mara ya mwisho Trump kufanya kikao na wanahabari ilikuwa mwezi Julai

Rais mteule, Donald Trump anatarajiwa leo Jumatano kufanya kikao na wanahabari baada ya karibu miezi 6 ikitarajiwa kuwa atakumbana na maswali kadhaa na hasa kuhusu madai kutoka kwa idara za upelelezi za Marekani kuwa Russia iliingilia uchaguzi alioshinda mwezi Novemba, na jinsi atakavyotenganisha bishara zake binafsi na kazi za urais.

Mara ya mwisho Trump kufanya kikao na wanahabari ilikuwa mwezi Julai ambapo alimshambulia mpinzani wake wa kutoka chama cha Demokratik, Hillary Clinton kwamba alichukua miezi kabla ya kuzungumza na wanahabari.

Marais wengi wa Marekani hutoa hotuba kwa wanahabari muda mfupi baada ya kuchaguliwa kinyume na Trump ambaye amekuwa akitumia akaunti yake ya Twitter na ujumbe mfupi lakini hajakutana rasmi na kundi la wanahabari kujibu maswali.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG