Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 00:59

Wademokrat Marekani wanafungua mkutano wao mkuu wa uteuzi Philadelphia


Mgombea wa chama cha demokratik Hillary Clinton gakizungumza na wafuasi wake huko Florida Julai 22, 2016.

Wademokrat Marekani wanafungua mkutano wao mkuu wa uteuzi Jumatatu utakaomuidhinisha rasmi mgombea kiti cha rais kwa uchaguzi wa mwaka huu, waziri wa zamani wa mambo ya nje Hillary Clinton, lakini ukiwa umegubikwa na utata juu ya kashfa ya barua pepe zilizovuja na kufichua jinsi viongozi wa chama hicho walivyomkejeli na kuikosoa kampeni ya Seneta wa Vermont, Bernie Sanders.

Debbie Wasserman Shultz, kiongozi wa kamati ya kitaifa ya chama cha Demokratic na ambaye amelazimika kuachia madaraka jumapili kufuatia kashfa hiyo iliyowekwa wazi na mtandao wa Wikileaks juu ya takriban barua pepe 20,000 alizomewa jumatatu na wafuasi wa Sanders wakati alipozungumza na kundi la wajumbe kutoka jimbo lake la Florida ambako yeye ni mbunge lakini hakuzungumzia juu ya barua pepe.

Anatarajiwa kujiuzulu rasmi mara tu baada ya kumalizika kwa mkutano huo unaoanza leo katika mji wa Philadelphia.Sanders alitoa wito wa Wasserman Schultz kujiuzulu wadhifa wake kufuatia kashfa hiyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG