Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 23:23

Mkutano kuhusu udhibiti wa hali ya hewa unafanyika Congo-Brazzaville


Mfano wa mandhari katika misitu ya bonde la Congo. (Credit: ©Wild-Touch, Sarah Del Ben, 2012)
Mfano wa mandhari katika misitu ya bonde la Congo. (Credit: ©Wild-Touch, Sarah Del Ben, 2012)

Wakuu wa nchi watafanya mazungumzo mjini Brazzaville siku ya Jumamosi. Waandaaji wanasema viongozi kadhaa katika mataifa ya Afrika ikiwemo Kenya, Rwanda, Gabon, Togo, Guinea-Bissau na Comoro wanatarajiwa kuhudhuria, pamoja na mwenyeji wa mkutano huo Rais wa Congo, Denis Sassou Nguesso.

Miaka 12 baada ya mkutano wa kwanza, mkutano wa pili ulijikita katika mabonde matatu makubwa ya misitu ya kitropiki duniani ambayo ni muhimu kwa udhibiti wa hali ya hewa ulifunguliwa mjini Brazzaville leo Alhamisi.

Mkutano wa wataalamu wa mazingira umeanza katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, utaanza katika ngazi ya mawaziri hapo kesho Ijumaa.

Wakuu wa nchi watafanya mazungumzo mjini Brazzaville siku ya Jumamosi.

Waandaaji wanasema viongozi kadhaa katika mataifa ya Afrika ikiwemo Kenya, Rwanda, Gabon, Togo, Guinea-Bissau na Comoro wanatarajiwa kuhudhuria, pamoja na mwenyeji wa mkutano huo Rais wa Congo, Denis Sassou Nguesso.

Hata hivyo hakuna viongozi wa nchi kutoka mataifa ya Amazon au Asia watakaohudhuria mkutano huo.

Wanamazingira, wanasayansi, makundi ya kampeni, viongozi wa kisiasa na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wamekusanyika Brazzaville kujadili mazingira ya Bonde la Congo, Amazon na Borneo-Mekong-Kusini Mashariki mwa Asia.

Mabonde haya matatu makubwa ya misitu yanachangia asilimia 80 ya misitu ya kitropiki duniani na “robo tatu ya Biodiversity yake”, waziri wa mazingira wa Congo Arlette Soudan-Nonault hivi karibuni aliwaambia waandishi wa habari.

Waziri huyo alitabiri kwamba mkutano wa kilele wa Congo-Brazzaville utatoa “azimio kali la kanuni”, lenye lengo la “kuendeleza mchanganyiko huu wa mabonde matatu”.

Forum

XS
SM
MD
LG