Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 19:41

Mke wa Gadhafi akimbilia Algeria


Wanawake wakiandamana dhidi ya Moammar Gadhafi kwenye uwanja wa kijani in Tripoli, Libya, usiku wa Jumatatu Augusti 29 2011
Wanawake wakiandamana dhidi ya Moammar Gadhafi kwenye uwanja wa kijani in Tripoli, Libya, usiku wa Jumatatu Augusti 29 2011

Viongozi wa upinzani wameitaka Algeria kuwarudisha mke na watoto watatu wa kiongozi wa Libya Gadhafi waloingia Algeria Jumatatu

Habari kutoka Libya zinaeleza kwamba mke wa kanali Gaddafi, Safiya, binti yake Ayesha na watoto wa kiume Muhammad na Hannibal waliondoka Libya mapema Jumatatu na kuingia Algeria.

Aisha Gadhafi,
Aisha Gadhafi,

Balozi wa Algeria katika Umoja wa Mataifa amesema walipokelewa kwa misingi ya kibinadamu. Maafisa huko Algiers wanasema waliripoti taarifa hiyo kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la mpito la Libya

Hannibal Moammar Gadhafi,
Hannibal Moammar Gadhafi,

Viongozi wa upinzani wa Libya wamesema kuwapa hifadhi familia ya Gaddafi ni kitendo cha uchokozi, na wametaka warejeshwe nchini Libya.

Viongozi wa waasi hapo awali wameituhumu Algeria, taifa pekee la Afrika kaskazini ambalo halijatambua Baraza la Mpito la Taifa, kwa kumsaidia Gadhafi na kumpaytia wamamluki ili kukandamiza upinzani wa wananchgi. Algeria imekanusha madai hayo.

Mohammed Moammar Gadhafi
Mohammed Moammar Gadhafi

Kiongozi wa Libya Gadhafi hadi hivi sasa hajulikani alipo pamoja na vijana wake wengine. Maafisa wqa vyeo vya juu wawaasi walitangaza Jumatatu kwamba huwenda mtoto wa kiume wa Gadhafi, Khamis , mkuu wa kikosi maalum cha wanamgambo wa jeshi ameuliwa katika mapambano siku ya Jumamosi kusini mwa tripoli.

XS
SM
MD
LG