Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:53
VOA Direct Packages

Mkataba wa kulinda maji ya kimataifa ya bahari wapitishwa New York


Samaki waruka kwenye bahari.

Kwa mara ya kwanza mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa yamekubaliana kuhusu mkataba wa pamoja wa kulinda mazingira kwenye maji ya bahari ya kimataifa.  Hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa hapo awali ilikuwa vigumu kulinda sehemu hizo kutokana na sheria tatanishi.

Kongamano la Umoja wa Mataifa lililobuni sheria za kulinda bahari lilibuniwa 1994 kabla ya suala la umuhimu wa mazingira bora ya bahari kutiliwa mkazo. Makubaliano hayo yaliofikiwa mwishoni mwa wiki ndiyo yalikuwa kilele cha kongamano la wiki mbili mjini New York.

Sheria za kulinda mazingira kwenye maji ya bahari ya kimataifa nje ya mipaka ya nchi zimekuwa zikijadiliwa kwa zaidi ya miaka 20 bila mafanikio yoyote. Makubaliano hayo ya Jumamosi jioni sasa yatatoa nafasi ya kulinda maji hayo ambayo ni karibu nusu ya eneo lote la dunia.

Nichola Clark ambaye ni mtaalam wa bahari kutoka taasisi ya Pew Charitable Trusts, na aliyekuwepo wakati wa mazungumzo ya New York amesema kwamba hatua iliyopigwa katika kulinda maji ya bahari ni ya kihistoria, ukiwa ushindi mkubwa wa kimazingira.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG