Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:31

Mji wa Mariupol, Ukraine, unasubiri kama Russia itaheshimu ahadi zake


Wanajeshi wa Russia, walipokuwa Mariupol (REUTERS/Alexander Ermochenko)
Wanajeshi wa Russia, walipokuwa Mariupol (REUTERS/Alexander Ermochenko)

Mji wa kusini mwa Ukraine, uliozingirwa wa Mariupol, Ijumaa umesubiri kama Russia, itaheshimu njia ya masuala ya kibinadamu ambayo itaruhusu misaada kupita na kuruhusu raia kuondoka.

Msemaji wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu Ewan Watson, amesema kwamba wanaendelea kuwa na matumaini wakati wakielekea Mariupol, lakini hawana uhakika kama itatokea leo.

Misafara inasambaza misaada na mabasi ya kuwaondoa raia yalisimamishwa hapo Alhamisi na vikosi vya Russia.

Mwanadiplomasia mkuu wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu, amesema katika mahojiano ya televisheni hapo Alhamisi kwamba Uturuki inafanya kazi kuzirejesha pande zote mbili kwenye meza ya mazungumzo.

Mkuu wa ujumbe wa Ukraine, David Arakhamia, amesema mazungumzo yataanza Ijumaa kwa njia ya mtandao.

Afisa wa kikanda wa Russia amesema Ukraine imefanya mashambulizi ya helikopta katika hifadhi ya mafuta Ijumaa katika mji wa Russia, Belgorod.

XS
SM
MD
LG