Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 03:53

Mjadala unaendelea kunusuru kufungwa serikali ya Marekani


Spika wa bunge la Marekani, John Boehner kutoka Republican akizungumza na wajumbe wenzake kuchukua hatua rahisi ili kuepuka kufungwa ofisi za serikali
Spika wa bunge la Marekani, John Boehner kutoka Republican akizungumza na wajumbe wenzake kuchukua hatua rahisi ili kuepuka kufungwa ofisi za serikali
Baraza la Seneti la Marekani linakutana Jumatatu kujaribu kufikia makubaliano na wabunge juu ya mswaada wa matumizi kabla ya kufikia muda wa mwisho saa 5 na dakika 59 usiku kuepuka uwezekano wa kufungwa kwa ofisi za serikali ya Marekani.

Wabunge wa chama cha Republican wanasisitiza kwamba hatua zozote za kuchelewesha au kupinga utiaji saini wa sheria ya huduma ya afya ya Rais Barack Obama yenye nia ya kutoa huduma kwa mamilioni ya wamarekani wasio kuwa na bima ya afya.

Kiongozi wa baraza la seneti, Harry Reid anaahidi kwamba mswada wa matumizi uliopitishwa na wabunge Jumamosi asubuhi ambao utachelewesha kwa muda wa mwaka mmoja sehemu muhimu za vipengele vya bima nafuu ya huduma ya afya, ijulikanayo kama Obamacare hautaidhinishwa.

Hatua hiyo imeonesha migawanyiko mikubwa kati ya wanasiasa wa chama cha Republican na Democratic.

Wa-democrat wanasema huduma ya afya ya Obamacare ni sheria ya nchi. Inawapa fursa watu wenye kipato kidogo na watu wasio na bima ya afya fursa ya kununua bima kwa gharama ya chini, serikali inapunguza makali ya sera hivyo basi familia hizo hazitakabiliwa na upungufu wa fedha iwapo kunatokea magonjwa makubwa sana.

Wa-republican wanasema program hiyo ya huduma ya afya inachanganya na haijakamilika. Pia wanasema kwamba sheria iliyopo kwenye mpango wa bima ya afya inaumiza uchumi wa nchi kwa kuweka kodi zaidi na kuwalazimisha wafanya biashara wadogo kutoa bima kwa waajiri wao.

Bwana Obama anasema hatokubali sheria ibadilishwe kwenye mpango wa huduma ya afya ya Obamacare.

Kama hakuna jambo lolote litakalopitishwa na wawakilishi wote katika baraza la seneti na bunge ifikapo jumatatu saa 5 na dakika 59 usiku, huduma zote za serikali zitaanza kufungwa isipokuwa zile muhimu sana. Huduma za watalii wanaokwenda kwenye bustani za kitaifa na nyumba za maonesho ya kumbukumbu ya kale zitafungwa. Mtu yeyote anayehitaji huduma ya hati ya kusafiria yaani passport au msaada wa kodi atatakiwa kusubiri. Zaidi ya wafanyakazi milioni moja huwenda wasipate mishahara yao katika kipindi cha kufungwa kwa ofisi zinazotoa huduma za serikali.
XS
SM
MD
LG