Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 04:09

Mivutano ipo juu kati ya Sudan na Sudan Kusini


Jeshi la serikali ya Sudan Kusini katika jimbo la Unity State
Jeshi la serikali ya Sudan Kusini katika jimbo la Unity State

Sudan Kusini inamshutumu jirani yake Sudan kwa kufanya mashambulizi ya anga katika mpaka wan chi hiyo na kuwajeruhi watu wasiopungua sita.

Maafisa wanasema ndege za kivita za Sudan zilishambulia wilaya ya Maban katika jimbo la upper Nile hapo Jumatano pia kulishambulia jimbo lake la Blue Nile mahala ambako serikali ya Khartoum inapambana na waasi tangu mwaka 2011.

Jimbo la Upper Nile ni makazi ya Zaidi ya wakimbizi 100,000 ambao wameyakimbia mapigano huko Blue nile.

Shirika la habari la Ufaransa-AFP linamkariri msemaji wa jeshi la Sudan kanali Al-Sawarmy Khaled akikanusha Sudan kushambulia sehemu yeyote ya eneo la Sudan Kusini.

Watoto waliokoseshwa makazi kutokana na mapigano
Watoto waliokoseshwa makazi kutokana na mapigano

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika-VOA msemaji wa jeshi la Sudan Kusini kanali Philip Aguer alisema shambulizi lilifanyika na alikanusha shutuma kutoka Khartoum kwamba Sudan Kusini inawasaidia waasi.

Alisema kwamba kwa sababu Sudan inaamini vingine, huwenda ikaishambulia Upper Nile kama ilikuwa inawasaka waasi ambao wanakatisha mpaka.

Mivutano kati ya Sudan na Sudan Kusini bado ipo juu tangu kusini ijitenge kutoka kaskazini na kuwa taifa huru mwaka 2011.

Nchi hizo mbili zinapigana juu ya masuala ya mpaka na mafuta na zinashutumiana kila mmoja kwa kuwasaidia waasi kwenye maeneo yao.

XS
SM
MD
LG