Mgombea kiti wa chama cha Republican ambae hakuwa akitajwa sana Rick Santorum, kwa mshangao mkubwa wa wengi amechukua nafasi ya pili katika uchaguzi wa awali wa jimbo la Iowa, nchini Marekani.
Uchaguzi huo ulofanyika Jumanne katika utaratibu wa kumchagua mgombea atakae kiwakilisha chama cha Republican katika uchaguzi mkuu, ulikua na ushindani mkubwa hadi dakika ya mwisho pale Romney aliyekua wakati wote akitarajiwa kupata ushindi alishinda kwa tofauti ya kura nane.
Mgombea mwengine aliyefanya vizuri bila ya kutegemewa ni mbunge Ron Paul aliyetokea watatu na hivyo kubadilisha kabisa mashindano katika chama hicho cha kihafidhina katika kumchagua mgombea atakae pambana na rias Barack Obama katika uchaguzi wa rais baadae mwaka huu.