Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 25, 2026 Local time: 15:59

Misri yatangaza mgao wa umeme kutokana na joto kali

Minara ya umeme nchini Misri
Minara ya umeme nchini Misri

Waziri mkuu wa Misri Alhamisi ametangaza hatua kadhaa ikiwemo mipango ya mgao wa umeme, ili kupunguza matumizi ya nishati wakati nchi hiyo na eneo pana, wakikabiliwa na wimbi la joto kali.

Watumishi wa umma watafanyia kazi nyumbani siku moja kwa wiki katika jitihada za kupunguza gharama kwenye mitandao ya umeme ya ndani, Mostafa Madbouli alisema katika hotuba kwenye televisheni, wakati vipimo vya joto vinavyozidi nyuzi joto 45 vilirekodiwa katika baadhi ya maeneo ya nchi wiki hii.

Alithibitisha pia kwamba mipango ya mgao wa umeme iliyotangazwa na serikali wiki iliyopita itaendelea, huku wakazi wakionywa kutotumia lifti nyakati fulani za mchana.

Hatua ya wiki iliyopita ilizua ukosoaji mkubwa, huku watu wengi wakilalamika kwamba mgao huo, ambao unafanyika mara kwa mara nyakati za joto kali mchana, mara nyingi ukidumu kwa zaidi ya saa mbili kwa siku na unatokea baada ya muda uliopangwa.

Madbouti Alhamisi alisema mgao uliopangwa utadumu kwa saa moja au mbili kwa siku, akiongeza kuwa unafanyika wakati matumizi ya nishati yanaongezeka.

Waziri mkuu huyo aliwaagiza watumishi wa umma ambao hawashughuliki moja kwa moja na kutoa huduma kwa umma kuanza kufanyia kazi nyumbani kila Jumapili kwa mwezi kuanzia Agosti 6, na kuhimiza sekta ya kibinafsi kuchukua hatua kama hizo.

Forum

​
XS
SM
MD
LG