Ripoti hiyo imesema IMF haikuhitaji Misri kupunguza matumizi ya ruzuku ikiongeza kuwa mpango huo mpya unalenga kuimarisha mtandao wa ulinzi wa kijamii kwa raia.
Bodi ya wakurugenzi wa IMF iliidhinisha siku ya ijumaa msaada wa kifedha wa miezi 46 wa dola bilioni 3 kwa nchi hiyo yenye watu wengi zaidi katika ulimwengu wa kiarabu ikisema inachochea ufadhili wa ziada wa takriban dola bilioni 14.
Misri ilifanya majadiliano kuhusu mkopo wake wa hivi karibuni wa IMF huku kuzorota kwa uchumi kutokana na vita vya Ukraine kulizidisha uhaba wa fedha za kigeni uliotokana na nakisi kubwa ya biashara Misri.
Wachambuzi wanasema hatua hii itasaidia Misri kutekeleza mahitaji yake ya kifedha katika eneohusika kufuatia msaada huo.