Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:00

Msichana mwenye saratani ajishughulisha na ubunifu wa mitindo


Utafiti mdogo unapendekeza kuwa kutumia mafuta ya zeituni(Olive Oil) kunaweza kupunguza athari za saratani ya matiti.
Utafiti mdogo unapendekeza kuwa kutumia mafuta ya zeituni(Olive Oil) kunaweza kupunguza athari za saratani ya matiti.

Msichana Noa Sorrel mwenye umri wa miaka 11 ambaye aligunduliwa kuwa na matatizo ya saratani kwa takriban mwaka mmoja uliopita amekuwa akifanyiwa tiba ya mionzi. Hali hii imemfanya kubadili mwenendo wake wa kimaisha.

Noa anasema baada ya kugundulika kuwa ana uvimbe katika seli ya damu mwezi Januari mwaka huu. Alipatwa na khofu kubwa, lakini daktari alimueleza kwamba saratani aliyonayo inaweza kutibika, ingawa ini si jambo rahisi. Kwahiyo hakuwa na wasi wasi mkubwa sana kwasababu alipewa matumaini, lakini wasi wasi alikuwa nao lakini si kwa kiwango kikubwa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:59 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Noa wakati akipatiwa matibabu hayo ya mionzi aliona njia bora ni kujishughulisha na mambo mengine kama vile kujifunza kushona kazi ambayo alikuwa akiifanya bibi yake kabla ya kufariki mwaka jana.

“ nilipatiwa tiba ya mionzi kwa miezi mitatu. Na siku na chochote cha kufanya. Kwahiyo ingekuwa ni kukaa tu bila ya kazi, kama nisingeanza kushona,” Noa anasema.

Noa siku zote alikuwa na ndoto ya kuwa mwana mitindo na taasisi ya Make a Wish lilitimiza ndoto yake.

Kundi hilo lisilo la kiserikali linawapatia msaada watoto ambao wamekumbwa na maradhi na hivyo kuwasaidia kuwapatia fursa ya kufanya kile wanachotaka kufanya na hilo lilimpa Noa nafasi ya kuonyesha nguvu zake kwenye onyesho la LA Fashion.

Akitumia cherehani ya bibi yake aina ya Singer aliwashonea nguo marafiki zake na ndugu zake.

Hivi sasa Noa ana furaha kubwa kwa kupewa cherehani mpya na inamfanya awe na shughuli nyingi za kushona, kusoma na kubuni mitindo ya majira ya baridi.

XS
SM
MD
LG