Mashahidi wanasema milipuko miwili imetokea katika mji wa kati wa Nigeria wa Kaduna Jumanne ikiwa mmoja karibu na kambi ya jeshi.
Polisi walisema mlipuko mmoja ulitokea karibu na daraja na mwingine katika kambi ya jeshi ya kitengo cha ufundi nje kidogo ya Kaduna . Maafisa wanasema idadi ya waliojeruhiwa haijajulikana.
Polisi walikuwa wakichunguza ripoti kwamba mlipuko wa kwenye kambi ya jeshi ulisababishwa na mlipua mabomu wa kujitoa muhanga ambaye aliingiza gari mbele ya eneo la kuingilia.