Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 08, 2023 Local time: 07:21

Milipuko imeripotiwa Melitopol katika mji unaokaliwa kimabavu na Russia


Mfano wa eneo lililopata mlipuko huko Melitopol katika jamhuri ya watu wa Donetsk. Ukraine, Dec. 11, 2022.

Ripoti kama hizo zinasema kuwa Ukraine pia ililenga mkoa wa Crimea uliokamatwa na Russia kwa mashambulizi ya makombora ambapo ripoti za milipuko kadhaa pia zilifuata

Ripoti zimeibuka za milipuko kadhaa katika mji unaokaliwa kimabavu na Russia wa Melitopol katika Jamhuri ya Watu wa Donetsk iliyojitangazia utawala kufuatia ripoti za Ukraine zikiulenga mji huo unaokaliwa kwa mashambulizi ya makombora Jumamosi usiku.

Ripoti kama hizo zinasema kuwa Ukraine pia ililenga mkoa wa Crimea uliokamatwa na Russia kwa mashambulizi ya makombora ambapo ripoti za milipuko kadhaa pia zilifuata.

Ndege zisizo na rubani za Russia zilishambulia mji wa bandari wa kusini mwa Ukraine wa Odesa nyakati za asubuhi siku ya Jumamosi, na kuuacha mji huo na eneo jirani bila umeme, maafisa wa eneo hilo wamesema.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema takriban watu milioni 1.5 hawana umeme, na maafisa wa mkoa wamewataka wakaazi ambao nyumba zao zinategemea umeme kuondoka.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG