Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 18:47

Mfahamu Mike Pence mgombea mwenza wa Donald Trump


Mike Pence katika mkutano mkuu wa chama cha Republican huko Cleveland, Ohio, Julai 19, 2016.
Mike Pence katika mkutano mkuu wa chama cha Republican huko Cleveland, Ohio, Julai 19, 2016.

Mfahamu Mike Pence mgombea mwenza wa mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump.

  • Hivi sasa ni gavana wa Indiana, nafasi ambayo ameishikilia kwa takriban miaka mitatu.
  • Ni mconservative ambaye anapendelea kuwepo kwa serikali ndogo
  • Ana rekodi nzuri ya kupunguza kodi, hasa kwa biashara.
  • Ameunga mkono sera ambazo zimeonekana za “kibaguzi”, ikiwa ni pamoja na kusimamisha kwa muda ufadhili kwa makundi ambayo yanawasaidia wakimbizi huko Indiana, sheria ya kuruhusu biashara kuwanyima huduma mashoga, na kupinga kuwapatia makazi huko Indiana wakimbizi kutoka Syria.
  • Awali alikosoa wito wa Trump wa kutaka waislamu kupigwa marufuku kuingia Marekani na kumshambulia jaji ambaye alikuwa anasimamia kesi ya chuo kikuu cha Trump.
  • Alitumika kwa vipindi sita kwenye baraza la wawakilishi la Marekani tangu mwaka 2000.
  • Awali alimuidhinisha Seneta wa Texas, Ted Cruz wakati wa utaratibu wa awali wa chama cha Republican wa baadhi ya wanachama kuwania uteuzi wa kugombea urais; aliahidi kumfanyia kampeni Trump baada ya kupata uteuzi mwezi Mei.
  • Anawaunga mkono vikali wakristo wa dhehebu la injili pamoja na waconservative.
  • Alihitimu katika shule ya sheria kwenye chuo kikuu cha Indiana mwaka 1986.
  • Ni mumewa Karen Pence na baba wa watoto watatu.
XS
SM
MD
LG