Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 22, 2025 Local time: 02:54

Mike Pence kutangaza kuwania urais wa Marekani


Makamu wa rais wa zamani wa Marekani, Mike Pence, atazindua kampeni yake ambayo ilikuwa ikitarajiwa ya kuwania uteuzi wa chama cha Republikan kugombea urais wiki ijayo jimboni Iowa.

Kutokana na hili amekuwa mgombea mwingine katika uwanja mpana wa wale wanaowania uteuzi wa kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Republikan, na kumfanya awe mpinzani wa bosi wake wa zamani.

Pence atazindua kampeni zake mjini Des Moines Juni 7, ambayo ni tarehe yake ya kuzaliwa akifikisha miaka 64 kwa mujibu wa watu wawili wanaofahamu mipango yake ambao hawakutaka kutajwa.

Anatarajiwa pia kutoa ujumbe wa video ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wake.

Timu yake inaona upigaji kura wa mapema jimboni Iowa kuwa ni muhimu ili kumwezesha kupata ushindi, na washauri wanasema anapanga kufanya kampeni kwa nguvu kuwavutia wapiga kura wenye mrengo wa kidini ya kikristo ambao ni idadi kubwa ya wapiga kura wa chama cha Republikan.

Forum

XS
SM
MD
LG