Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 09, 2024 Local time: 13:09

Miili zaidi yapatikana baada ya shambulio la bomu lililoua zaidi ya watu 10 nchini Somalia


Jamaa wakisubiri miili ya ndugu zao kuondolewa kwenye jengo lililoharibiwa, siku moja baada ya shambulio la bomu lililotegwa kwenye magari mawili kwenye barabara yenye shughuli nyingi mjini Mogadishu, Oktoba 30, 2022.
Jamaa wakisubiri miili ya ndugu zao kuondolewa kwenye jengo lililoharibiwa, siku moja baada ya shambulio la bomu lililotegwa kwenye magari mawili kwenye barabara yenye shughuli nyingi mjini Mogadishu, Oktoba 30, 2022.

Wafanyakazi wa dharura katikati mwa Somalia walichimba kwenye vifusi ili kupata miili zaidi baada ya shambulio la bomu kwa kutumia lori dogo lililoua zaidi ya watu 10 na kusababisha majengo kuanguka.

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliendesha gari hilo lililokuwa limesheheni vilipuzi akilielekeza kwenye kituo cha ukaguzi wa usalama katika mji wa Beledweyne siku ya Jumamosi, na kusababisha mlipuko ambao ulipelekea watu wengi kukwama chini ya matofali.

Polisi wameliambia shirika la habari la AFP leo Jumapili kwamba idadi ya waliofariki imeongezeka na kuvuka vifo 13 vilivyoripotiwa awali lakini hawakutoa idadi kamili.

“Operesheni ya kutafuta na kusafisha imeendelea kwenye eneo la mlipuko na maiti zilipatikana Jumapili asubuhi chini ya vifusi vya baadhi ya majengo,” amesema Sayid Ali, naibu kamanda wa kituo cha polisi cha Beledweyne.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud alilaani shambulio hilo, lakini alionekana kubadili kauli juu ya azma yake ya “kuwatokomeza” wanamgambo wa Al-Shabab ambao wameendesha uasi dhidi ya serikali kuu tete ya nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 15.

Alisema “ Matukio kama haya hayatatuvunja moyo kamwe kwa kuendelea na harakati za kuwatokomeza magaidi.”

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio la Jumamosi.

Forum

XS
SM
MD
LG