Waathirika wa maporomoko makubwa ya matope yaliyosababishwa na dhoruba katika kijiji cha pwani ya Ufilipino ambacho wakati mmoja kilikuwa kimeharibiwa na tsunami, kwa bahati mbaya walidhani mawimbi yalikuwa yanakuja na hivyo kukimbilia eneo la nyanda za juu ambako walifukiwa wakiwa hai na mapromoko hayo, afisa mmoja alisema Jumapili.
Takriban miili 18, ikiwa ni pamoja na ya watoto, imefukuliwa na waokoaji katika eneo ambalo hivi sasa matope yamefunika sehemu kubwa ya kijiji cha Kusiong, katika jimbo la kusini la Maguindanao, miongoni mwa maeneo yalioathiriwa vibaya sana na dhoruba ya kitropiki la Nalgae, ambayo ililikumba eneo la kaskazini magharibi mwa Ufilipino mapema Jumapili.
Maafisa wanahofia watu 80 hadi 100 zaidi, ikiwa ni pamoja na familia nzima, huenda walifukiwa au kusombwa na mafuriko huko Kusiong, kati ya Alhamisi usiku na mapema Ijumaa, kulingana na Naguib Sinarimbo, waziri wa mambo ya ndani wa jimbo linalojitawala la Kiislamu linaloendeshwa na wapiganaji wa zamani wa msituni waliokuwa wanataka kujitenga.