Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 16:17

Miili 28 imegunduliwa Burkina Faso;Polisi nchini humo imethibitisha


Ramani ya Burkina Faso
Ramani ya Burkina Faso

Mashambulizi yanayolenga vikosi vya usalama na raia yameongezeka katika miezi ya karibuni, hasa katika mikoa ya kaskazini na mashariki inayopakana na Mali na Niger, ambayo pia inapambana na wanajihadi

Miili 28 iligundulika kaskazini magharibi mwa Burkina Faso mwishoni mwa wiki serikali imesema, ikieleza uchunguzi unaendelea huku uvumi ukiongezeka kuhusu nani huendakuhusika.

Mashambulizi yanayolenga vikosi vya usalama na raia yameongezeka katika miezi ya karibuni, hasa katika mikoa ya kaskazini na mashariki inayopakana na Mali na Niger ambayo pia inapambana na wanajihadi.

Serikali ilifahamishwa kuhusu tukio la Nouna. wakati wa usiku wa Desemba 30-31," taarifa ya serikali ilisema Jumatatu jioni.

Ripoti za awali "zinaonyesha watu 28 waliuawa," ilisema, na kuongeza kuwa uchunguzi umefunguliwa na kusihi kuwepo na utulivu.

Shirika la CISC (Collective of Communities against Impunity and Stigmatisation) lilishutumu vurugu hizo kama "visasi vinavyowalenga raia" na raia wenye silaha wanaodai kuwa wanachama wa kikosi saidizi cha VDP ambao "wanajihusisha kwa uhuru katika uporaji uliopangwa na kulenga unyanyasaji wa raia."

Moja ya nchi masikini sana duniani, Burkina Faso tayari imeshuhudia mapinduzi mawili yaliyofanywa na maafisa wa jeshi wasioridhika mwaka huu ambayo yameliweka jeshi madarakani.

XS
SM
MD
LG