Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 11:47

Miguna Miguna aondolewa kwa nguvu nchini Kenya.


Miguna Miguna

Kwa mara nyingine tena serikali ya kenya imekaidi amri ya mahakama kuu iliyoitaka kumuachia wakili na mwanaharakati wa kisiasa Miguna Miguna, ambaye alikuwa amezuiliwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta JKIA kwa zaidi ya saa 24.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya mmoja wa mawakili wa bwana Miguna, Nelson Havi amethibitisha kwamba mteja wake aliingizwa kwa nguvu kwenye ndege ya shirika la ndege la Emirates iliyokuwa inaelekea Dubai. Miguna alizuiliwa JKIA baada ya kuwasili kutoka Canada ambapo awali alirejeshwa huko kwa madai kuwa alikuwa ameukana uraia wa kenya. Tangu kuwasili nchini Kenya wakili Miguna alinyimwa ruhusa ya kuingia nchini humo licha ya amri mbili za mahakama kuelekeza arejee nchini kwa vile kufukuzwa kwake nchini Kenya na kupelekwa Canada kulifanyika kinyume cha sheria.

katika taarifa ya awali aliyoitoa jana bwana Miguna alisema alikuwa amezuiliwa kwenye chumba kidogo bila ya kupatiwa huduma za msingi ambazo ni muhimu kwa maisha ya mwanadamu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG