Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 04:05

Kongamano la uhamiaji la Umoja wa Ulaya na Africa lafanyika Malta.


Viongozi wa Africa na Ulaya wakiwa kwenye mkutano juu ya uhamiaji huko Malta , Italy
Viongozi wa Africa na Ulaya wakiwa kwenye mkutano juu ya uhamiaji huko Malta , Italy

Mohamadou Issoufou, rais wa Niger, alisema, Euro bilioni 1.8 hazitoshi. Hata hazikaribii kutosha. Mahitaji ni mengi. Ndio maana tunasihi washirika wote kuhusika katika kutoa misaada.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:53 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Katika kongamano lililofanyika Malta kati ya viongozi wa Ulaya na Afrika, umoja wa ulaya umekubali kutoa msaada wa dola bilioni 1.9 kwa lengo la kukabiliana na tatizo la uhamiaji. Maelfu ya watu wamevuka bahari ya Mediterranean mwaka huu kiasi cha kupita uwezo wa mataifa ya ulaya kukabiliana na janga hilo.

Mwezi Aprili karibu watu 800 walikufa maji wakijaribu kuingia Ulaya. Miili yao ilisafirishwa na maji hadi kwenye ufukwe wa Malta. Janga hilo limepelekea mkutano wa wiki hii huko Malta ambapo viongozi wa Ulaya wametia saini mkataba wa dola bilioni 1.9 kwa Afrika lengo kuu likiwa ni kukabiliana na kile walichokitaja kuwa ‘kiini hasa cha uhamiaji’. Fedha hizo zinalenga kutengeneza ajira, kuimarisha hali ya afya na kuzuia mizozo. Viongozi wa ulaya walitoa mkakati ulio chapishwa kwenye kurasa 17 wa kukabiliana na mzozo ulioko ingawa ulipokelewa kwa maoni tofauti. Kama anavyosema rais wa Niger Mohamadou Issoufou.

Mohamadou Issoufou, rais wa Niger, alisema, Euro bilioni 1.8 hazitoshi. Hata hazikaribii kutosha. Mahitaji ni mengi. Ndio maana tunasihi washirika wote kuhusika katika kutoa misaada.

Nae waziri mkuu wa Italy , Matteo Renzi alisema, haya ni maamuzi kutoka kwa wale wanaoona kikombe kikiwa tupu nusu. Kwangu naona kikombe kikiwa zaidi ya nusu kujaa kwa sababu mwanzo, Italy haiku peke yake katika kukabiliana na wakimbizi, pili, Afrika imepewa kipaombele.

Lakini hesabu hizo zinaonyesha kuwa afrika haijapewa kipaombele kama anvyoeleza Marta Foresti kutoka taasisi ya maendeleo ya nchi za ulaya anasema,Euro bilioni 3 ziliahidiwa uturuki ili kusaidia kukukabiliana na hali huko Syria. Kwa hivyo tunaangalia kwa mtazamo huo na kulinganisha, dola bilioni 1.9 kwa bara lote la Afrika hazitoshi.

Ulaya pia inanuiya kutia saini mikataba ya uhamiaji na mataifa binafsi ya Afrika kabla ya kutoa misaada ya maendeleo.

Hata hivyo , idadai ya wanaovuka Medditeranean ni ndogo ikilinganishwa na ile ya zaidi ya wahamiaji 650,000 wengi wakiwa ni kutika Syria wakipitia Uturuki na Ugiriki.

Sweden ambayo kwa muda mrefu imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono haki za wahamiaji imeingia kwenye mataifa ambayo yameanza tena kutoa hati za kuingia (VISA) wiki hii kama avyosema waziri mkuu swa Sweden Stefan, anasema,tunafuata sheria zilizowekwa hapa ulaya, tunafanya hivyo kwa kuwa mamlaka zinasema hatuwezai kuhahakikisha usalama kwenye mipika yetu, lazime tusikilize hilo

Waangalizi wanasema hatua ya Sweden inaongeza tashwishwi kuhusu eneo lisilo hitaji kibali kuingia Ulaya katika siku zijazo.

XS
SM
MD
LG