Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 20:13

Mwanamke wa Kipalestina auwawa


Jeshi la Israel limesema kuwa mwanamke wa kipalestina aliejaribu kushambulia mwanajeshi kwa kisu ameuwawa kwa kupigwa risasi mapema leo.

Shambulizi hilo ni la karibu kabisa kuwahi kutokea kati ya mengine mengi ambayo yamekuwa yakitokea tangu mwezi Oktoba mwaka jana na ambayo yameuwa wapalestina 206 pamoja na waisraell 28.

Kulingana na mamlaka za Israel, wengi wa wapalestina waliouwawa walikuwa wakishambulia kwa kutumia visu au bunduki.

Mashambulizi hayo hata hivyo yamepunguka katika wiki za karibuni. Mapema wiki hii, mvulana wa kipalestina mwenye umri wa miaka 17 alikamatwa Tel Aviv baada kumchoma mwanajeshi kisu.

XS
SM
MD
LG