Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 11:33

Mifumo ya teknolojia ya NAVY yashambuliwa


Mashambulizi ya mitandao
Mashambulizi ya mitandao

Jeshi la majini nchini Marekani lilisema wezi wa shambulizi la mitandao wamepata fursa ya kuingia kwenye mtandao wa namba nyeti binafsi za mtu-Social Security inayoweza kukupatia taarifa kamili za mtu na taarifa nyeti nyingine kwa zaidi ya wafanyakazi 134,000 waliopo kazini na wa zamani wa jeshi la majini Marekani.

Uvujaji wa takwimu ulitokea baada ya wezi wa mitandao kuingia kwenye laptop za mkandarasi Hewlett Packard Enterprise mwajiriwa wa Navy. Katika taarifa iliyotolewa Jumatano, Navy ilisema taarifa hizo zilichukuliwa na watu wasiojulikana na kwamba uchunguzi unafanyika ili kutambua na kuwasaidia watu ambao taarifa zao zimevuja.

XS
SM
MD
LG