Ameongeza kuwa jeshi la Ukraine bado linadhibiti sehemu muhimu katika pande zote.
Miezi tisa ya uvamuzi wa Ukraine imetimia huku sehemu kubwa ya Ukraine ikiwa katika giza bila huduma ya maji safi kutokana na mashambulizi makali ya makombora ya Russia dhidi ya miundombinu ya kiraia, ambayo yalikata umeme nchini kote tarehe 23 Novemba.
“Kwa pamoja tumevumilia miezi tisa ya vita kamili na Russia haijapata njia ya kutuvunja nguvu, na haitoipata,” Zelenskiy amesema.
Amesema vikosi vya Russia vimekuwa vikiushambulia vikali mji wa Kherson, ambapo vikosi vilivyokuwa vinaukalia mji huo viliondoka mapema mwezi huu.
Amesema Kherson ndio mji pekee ambao walifaulu kuuteka katika uvamizi wao wa miezi tisa kamili.