Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 19:09

Michelle Obama atoa wito duniani kusaidia wasichana kusoma


Michelle Obama katika kampeni ya Let Girls Learn.

Mke wa Rais Barack Obama wa Marekani, Bi. Michelle Obama, alitoa wito Kwa jamii ya kimataifa kusaidia wasichana kote ulimwenguni kuondoa vizuizi ili kupata elimu wanayoihitaji kuweza kuendesha maisha yao.

Wito wa bi. Obama umekuwa kwenye siku ya msichana kimataifa, iliyoanzishwa na kikao cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2011, kutambua haki za wasichana na changamoto za kipekee wanazokabiliana nazo wasichana kote duniani.

Katika tangazo la kwenye mtandao wa cnn.com Michelle alitoa wito wa uungwaji mkono wa kampeni za “Let Girls Learn” juhudi za dunia kuhamasisha elimu kwa wasichana ambao hawapo shule.

Michelle Obama alirudia kusema matarajio ya juhudi zake yamekuja baada ya miaka miwili iliyopita alipokutana na msichana Malala Yousafzai raia wa Pakistan ambaye alifyatuliwa risasi kichwani na wanamgambo wa kundi la Taliban nchini Pakistan kwa kujaribu kuhudhuria shule.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG