Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 03:28

Michele Obama atafanyia kampeni Clinton jimboni Arizona


Mgombea urais Marekani kwa chama cha Democratic, Hillary Clinton
Mgombea urais Marekani kwa chama cha Democratic, Hillary Clinton

Mgombea kiti cha rais wa chama cha Democratic Hllary Clinton akizidi kua na matumaini ya kushinda uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba, na kumzuia mpinzani wake Donald Trump kupata ushindi ameamua kupanua kampeni yake kwa kuingia majimbo yanayo kwa kawaida yanadhibitiwa na chama cha Republican.

Akifanya hivyo anawasaidia pia wagombea viti vya bunge la taifa wa chama chake kupata ushindi. Huku zikiwa zimebaki wiki tatu hadi siku ya uchaguzi kampeni ya Clinton inasema itatumia zaidi ya dola milioni mbili za matangazo katika jimbo la Arizona ambalo limepiga kura kwa rais mdemocratic mara moja peke yake katika uchaguzi 16 zilizopita.

Michelle Obama
Michelle Obama

Pia kampeni inapanga kumpeleka mmoja ya wafuasi wake maarufu, Michelle Obama kwenye jimbo hilo siku ya Alhamis kufanya mkutano wa kampeni kwa Clinton.

Uchunguzi wa maoni wa karibuni unaonesha Clinton na Trump wako sare katika kinyang’anyiro kwenye jimbo la Arizona lililopo kaskazini na mpaka wa Mexico.

XS
SM
MD
LG