Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 03:54

Michael Phelps aendeleza rekodi


Mwogeleaji kutoka nchini Marekani, Michael Phelps anaendelea kuweka rekodi baada ya Jumapili usiku kushinda medali ya 23.

Kabla mashindano haya ya Olympic kwa mwaka huu wa 2016, Phelps tayari alikuwa anashikilia rekodi ya kuwa na medali nyingi za Olympic kuliko mwanamichezo yoyote duniani.

Licha ya ushindi wa jana wa medali ya 19 ya dhahabu, wachambuzi wanasema kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza medali zaidi katika mashindano mengine ya Olympic hii.

Phelps mwenye miaka 31, alishinda medali ya dhahabu na wanamichezo wenzake watatu Caeleb Dressel, Ryan Held, na Nathan Adrian na kuwa na idadi ya jumla ya medali 23.

Ushindi huo ulitokana na kuogelea kwa muda wa dakika 3 na sekunde 9.92. Michael Phelps alipata medali ya kwanza ya dhahabu kwa mwaka huu, na anaendelea kuwa mwanamichezo bora wa Olympic wa muda wote kwa sasa.

XS
SM
MD
LG