Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 07:46

Miaka 20 baada ya mauwaji ya halaiki ya Rwanda


Kikao cha mahakama ya kijadi Gacaca iliyokua na jukumu la kuwahukumu walohusika na mauwaji ya halaiki ya 1994, Rwanda (Archives)
Kikao cha mahakama ya kijadi Gacaca iliyokua na jukumu la kuwahukumu walohusika na mauwaji ya halaiki ya 1994, Rwanda (Archives)
Viongozi, waatalamu na wageni wa heshima kutoka shemu mbali mbali za dunia wako Rwanda kuhudhuria maadhimishi ya miaka 20 tangu kutokea mauwaji ya haliki yaliyosababisha vifo vya karibu watu laki nane, yanayoanza rasmi Jumatatu.

Akizungumza katika kuufunga mkutano wa kimataifa wa siku tatu juu ya mauwaji ya halaiki, mjini Kigali Jumapili, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo, alirudia tena matamshi ya rais Paul Kagame kwamba Ufaransa ilihusika katika matayarisho ya mauwaji hayo kwa kiasi fulani.

Rais Kagame alitoa matamshi hayo alipohojiwa na Jarida la Jeune Afrique, akisema kwamba Ufaransa na Ubelgiji zilihusika moja kwa moja katika maandalizi ya kisiasa ya mauaji hayo ya 1994.
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:36 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Matamshi hayo ya rais Kagame yalipelekea Ufaransa kuvunja mipango ya kushiriki kwenye maadhimisho hayo wiki hii na msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Ufaransa alisema matamshi hayo ni ya kusikitisha na yanakwenda kinyume na utaratibu unaoendelea hivi sasa wa kurudisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Kigali, Sylvanus Karemera anasema ingawa kuna baadhi ya viongozi wa upinzani wanaoishi uhamishioni anadai hakuna maeneleo yaliyiopatikana, lakini Wanyarwanda wengi wanahisi utaratibu wa upatanishi umepiga hatua kubwa sana.

Anasema "hivi sasa imani imeanza kurudi na watu wanashuhudia ndoa za mchanganyiko zikifanyika tena kati ya Wahutu na Watutsi. Anaongeza kusema kuna juhudi nyingi za upatanishi na maridhiano zinazoendelea nchini humo.
XS
SM
MD
LG