Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:25

Miaka 11 ya program ya DACA ya Marekani mustakbali wake bado hauna uhakika


Immigration Deferred Action

Majimbo yanayoongozwa na chama cha Republican yanatoa changamoto mahakamani kwenye program hii maarufu DACA kwa lengo la kuisitisha. Jaji wa mahakama moja ya Marekani Andrew Hanen wa Wilaya ya Kusini mwa jimbo la Texas alisikiliza hoja hapo Juni Mosi huko Texas dhidi ya Marekani

Sera ya serikali kuu ambayo inalinda dhidi ya kuwarudisha nyumbani maelfu kwa maelfu ya wahamiaji walioletwa Marekani wakati wakiwa watoto imetimiza miaka 11 siku ya Alhamisi. Lakini mustakbali wa programu hiyo bado hauna uhakika kwa sababu ya mapambano ya miaka sita mahakamani.

Majimbo yanayoongozwa na chama cha Republican yanatoa changamoto mahakamani kwenye program hii maarufu DACA kwa lengo la kuisitisha. Jaji wa mahakama moja ya Marekani Andrew Hanen wa Wilaya ya Kusini mwa jimbo la Texas alisikiliza hoja hapo Juni Mosi huko Texas dhidi ya Marekani.

Mwaka 2021 Hanen aliamua kuwa DACA ilikuwa kinyume cha sheria kwa sababu haikuwa chini ya ilani ya umma na kipindi cha maoni ambacho kinahitajika chini ya Sheria ya Utaratibu katika Utawala wa serikali kuu.

Mwaka 2022 Idara ya Usalama wa Nchi ilitoa sheria mpya ya kuimarisha program hiyo, kwa kutumia taarifa ya umma na kipindi cha maoni. Hanen anaangalia uhalali wa sheria hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG