Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 10:23

Mahujaji wamiminika Mecca


Picha ya mahujaji wakizunguka Kaaba Jumatano

Kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili, mji mtakatifu wa Mecca, Saudi Arabia umeanza kuonyesha dalili ya kurejea kwenye hali ya kawaida.

Hilo linafanyika wakati mahujaji takriban milioni 1wanapofanya ibada ya hijja tangu kuzuka kwa janga la corona lililopelekea mataifa mengi kufunga mipaka yao. Mahujaji wamekusanyika mapema leo kwa sala za kwanza ikiwa nguzo muhimu kwenye dini ya kiislamu.

Mahujaji hutumia siku kadhaa kwenye maeneo takatifu wakati wakitumia mapito yanayoaminika kutumiwa na mtume Muhammad takriban miaka 1,400 iliyopita. Moja wapo ya tamaduni muhimu ni kuzunguka Kaaba ambapo ni mahala patakatifu zaidi katika dini ya kiislamu. Hijja ni nguzo muhimu kwa kila muislamu mwenye uwezo wa kifedha na kimwili walao mara moja maishani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG