Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:54

Mgonjwa wa Mwisho wa Ebola huko Sierra Leone atoka Hospitali


Adama Sankoh, mbele akiwa amesimama na maafisa wa afya.
Adama Sankoh, mbele akiwa amesimama na maafisa wa afya.

Maafisa wa afya huko Sierra Leone wamemuachilia mgonjwa wa mwisho kutoka hospitali Jumatatu ikiwa ni mwanzo wa siku 42 kwa nchi hiyo kutangazwa kutokuwa na Ebola tena.

Adama Sankoh aliondoka kutoka kituo cha tiba ya Ebola kilichoko kwenye kitongoji cha mji wa Makeni baada ya kupokea matokeo ya pili yaliyoonyesha kuwa hana virusi vya Ebola.

Maafisa walifanya sherehe iliyohudhuriwa na Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone. Sankoh ambaye mtoto wake wa kiume alikufa kutokana na Ebola aliwashukuru wafanyakazi wa afya kwa msaada wao wakati alipokuwa mgonjwa.

Ugonjwa wa Ebola umeathiri Afrika Magharibi kwa zaidi ya miezi 18 na umeambukiza zaidi ya watu 28,000 wengi wakitokea nchini Sierra Leone, Liberia na Guinea.

Zaidi ya watu 11,200 wamekufa kutokana na Ebola 4,000 miongoni mwao wakiwa ni kutoka Sierra Leone.

XS
SM
MD
LG