Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 23:02

Mgomo wa wachimba madini wapamba moto Afrika Kusini


Wachimbaji madini wakiwa katika mgomo Afrika Kusini
Mgomo wa wachimba migodi huko Afrika Kusini unaendelea kukiwepo na mikutano ya hadhara inayohutubiwa na wanaharakati wa kisiasa wanaotetea maslahi ya wachimbaji hao
.
Katika hotuba ilitolewa na mwanasiasa maarufu Julius Malema na kushangiliwa na wachimbaji wa madini wanaogoma wakipiga filimbi na vuvuzela, alitoa mwito wa kuwepo na mgomo wa kitaifa katika migodi yote ya nchi hiyo, akishawishi kuimarishwa kwa mgomo ambao tayari umesitisha uzalishaji wa madini katika migodi ya platinum na dhahabu.

Kilomita 100 kutoka mahali walipo wafanyakazi wa migodi elfu 8 wanaogoma na wafuasi wao huku wakizingirwa na polisi waliokuwa kwenye magari yenye silaha na helikopta waliandamana hadi hospitali moja kuwatembelea wachimba madini wenzao 190 ambao wanasema walipigwa na kuteswa katika jela ya polisi.

Mlinzi wa kampuni ya madini aliyevalia koti la kujikinga na risasi aliwaambia waandishi wa habari kuwa wagonjwa waliondolewa kutokana na sababu za kiusalama huku kundi kubwa la polisi likizuiya waandamanaji hao kuingia hospitali.
XS
SM
MD
LG