Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:43

Mgombea Ubunge Tanzania Deo Filikunjombe afariki


Polisi katika eneo la ajali ya chopa ya Filikunjombe
Polisi katika eneo la ajali ya chopa ya Filikunjombe

Deo Filikunjombe aliyekuwa anatetea jimbo lake la LUDEWA kwa tiketi ya CCM anakuwa mbunge wa sita kupoteza maisha katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu na hivyo utalazimu pia uchaguzi wa ubunge kuahiriswa kwenye jimbo hilo.

Kamishna wa operesheni na mafunzo wa Jeshi la polisi, nchini Tanzania Paul Chagonja amethibitisha kutokea kwa ajali ya helikopta Nnamba 5YDKK katika eneo la pori la selou kwenye kijiji cha Mtende mkoani Morogoro iliyosabaaisha vifo vya watu wanne akiwemo mgombea wa ubunge jimbo la Njombe Deo Filikunjombe.

Akizungumza na Sauti ya Amerika kwa njia ya simu tokea eneo la tukio kamishna Chagonja amesema maiti nyingine iliyotambulika ni ya rubani wa helikopta hiyo William Slaa huku abiria wengine wawili ambao ni wanaume wakiwa bado hawajatambulika.

Filikunjombe ambaye alihitimu shahada ya uandishi katika chuo kikuu cha Makerere Uganda amewahi kufanya kazi katika vyombo vya habari nchini Tanzania kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Ludewa katika uchaguzi wa mwaka 2010.

Mbunge mwingine afariki kwa ajali Tanzania
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:39 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Taarifa za kuanguka kwa helikopta iliyopoteza uhai wa Filikunjombe aliyekuwa mbunge machachari na makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali katika bunge lililopita zilianza kusambaa Alhamisi jioni katika mitandao mbalimbali ya kijamii na hatimaye majira ya mchana Ijumaa ndio ikathibitika kwamba watu wote waliokuwemo kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia

Kamishna Chagonja amesema polisi na taasisi nyingine ikiwemo mamlaka ya usalama wa anga imeanza uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya helikopta ambayo inadaiwa ilikuwa imekodiwa na marehemu Deo Filikunjombe

Deo Filikunjombe anakuwa mbunge wa sita kupoteza maisha katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu na hivyo utalazimu pia uchaguzi wa ubunge kuahiriswa kwenye jimbo hilo.

XS
SM
MD
LG