Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:58

Mgogoro wa Misri waendelea


Wafuasi wa Mohammed Morsi wakionyesha picha yake katika mji wa Nasr Julai 27,2013
Wafuasi wa Mohammed Morsi wakionyesha picha yake katika mji wa Nasr Julai 27,2013
Maafisa wa Misri na wafanyakazi wa afya wanasema dazeni za watu wameuawa katika mzozo baina ya maafisa wa ulinzi na wafuasi wa rais aliyetimuliwa madarakani Mohammed Morsi lakini wafuasi wa Morsi wanasema idadi hiyo ni kubwa zaidi.

Watoa huduma za afya katika hospitali moja ya Cairo wamesema takriban watu 38 wameuawa katika mapigano.

Katika mji wa Alexandria, taarifa zinasema watu saba wameuawa tangu Ijumaa. Chama cha Morsi cha Muslim Brotherhood kinasema idadi ya waliouawa ni mara mbili ya idadi inayoelezewa na maafisa wa Misri.

Wahudumu katika hospitali hiyo mjini cairo wanasema wamelemewa kutokana na wingi wa majeruhi.

Hospitali hiyo imo katika kijiji cha Nasr kilichoko Cairo ambacho pia ni ngome ya kundi la Brotherhood , kijiji ambacho wafuasi wa Mosri wamepiga kambi kwa wiki tatu sasa.
XS
SM
MD
LG