Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:41

Mfanyakazi wa ndege ya Angola akwama kwenye mizigo


Mfano wa ndege TAAG Angola iliyolazimika kutua Lisbon
Mfano wa ndege TAAG Angola iliyolazimika kutua Lisbon

Ndege moja ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Ureno kwenda Angola ililazimika kutua kwa dharura huko Lisbon baada ya mfanyakazi mmoja wa huduma za mizigo kuripotiwa amepotea na baadae mtu huyo kupatikana ndani ya eneo la mizigo akiwa hai lakini anashindwa kupumua vizuri na joto lake la mwili likiwa limeshuka.

Msemaji wa uwanja wa ndege wa Lisbon, Rui Oliveira aliliambia shirika la habari la Associated Press-AP kwamba ndege ya shirika la ndege la TAAG Angola iliondoka mji wa Porto huko Ureno saa nne asubuhi kwa saa za huko siku ya Jumapili kuelekea mji mkuu wa Angola, Luanda.

Mfanyakazi huyo aliripotiwa kutoonekana kwenye uwanja wa ndege wa Porto baada ya kupakia mizigo na inaaminika alikwama ndani ya sehemu ya mizigo alisema msemaji huyo.

Ndege hiyo ilitua kwa dharura huko Lisbon mwendo wa saa tano asubuni kwa saa za huko. Oliveira hakuelezea taarifa zaidi kuhusu mfanyakazi huyo lakini alisema yupo katika hali ya kuridhisha na anapatiwa huduma katika hospitali moja mjini Lisborn.

XS
SM
MD
LG