Waziri wa mambo ya zamani wa Misri anasema leo Alhamisi kwamba picha za rada za maziko ya mfalme maarufu Tut zinaonyesha uwezekano wa kuwepo vyumba viwili vilivyofichwa ambavyo vinaweza kuwa na metali na vifaa vingine.
Mfalme Tut alifariki mwaka 1324 kabla ya Kristo na wataalam wa mambo ya zamani walishangaza dunia baada ya kugundua kaburi lake likiwa limejaa vitu vya thamani vya zamani mwaka 1922.
Mtalaam wa mambo ya zamani wa Uingereza anaamini kwamba chumba hicho kingine kitakuwa na mabai ya Malkia Neferiti mke wa baba wa Mfalme Tut.